Lister Elia.com

Welcome to Lister Elia's Official Web Site


MADA YA KI-TAALUMA KUHUSU MUZIKI.MCHANGO WA LISTER ELIA KWA WAPENDAO KUJIFUNZA ELIMU YA MUZIKI. 

Waungwana,kwa heshima na taadhima naleta hii mada inayohusiana na mambo ya utaalamu kuhusu tasnia ya muziki ambayo,ni kazi kama zilivyo kazi zingine zote.Nia hapa ni kumega kidogo nilichonacho/ninachokijua katika taaluma hii ili,
wenye nia ya kujifunza moja au mawili,waweze kufanya hivyo.

MUZIKI NI NINI?!.
Hili ndilo swali la kwanza la kujiuliza kwa yeyote anayetaka kuigusa nyanja hii
japo kwa kusoma kama historia na si kuingia katika mazoezi ya vitendo na 
hatimaye kuonesha kipaji chake mbele ya kadamnasi.

Hapa kila mtu anaweza kulijibu swali hili kulingana na utashi wake na uelewa alionao katika fani hii, kutokana na aliyoyaona na kuyasikia kuhusu muziki.Ikumbukwe kwamba,"sikio" ni kiungo muhimu katika mwili kinachoupokea mdundo
wa ngoma kwa namna ya kipekee, na kumfanya mlengwa aanze kutikisa viungo
vya mwili wake wakati mwingine pasipo mwenyewe kujijua.

Lakini kwangu mimi, kwa kutumia neno moja, nitasema.... muziki ni "SOUND"(MLIO). 
SOUND ndiyo inayotengeneza muziki,endapo sound hizo zitapangwa katika 
ufundi na umaridadi unaovutia masikioni mwa m/(wa)-lengwa.
SOUND hiyo hiyo,inaweza kuwa mbaya au "kelele" masikioni endapo mtumiaji
hakufanya kazi ya ziada kuzioanisha sauti ili ziwe burudani masikioni.

SOUND inaweza kutumika pia kama kiashirio cha tukio linalotegemea kutokea au
lililokwisha tokea.Mfano ni kama kengele zinazoashiria tukio la Ibada makanisani, matumizi ya ngoma vijijini tangu karne nyingi zilizopita,kama njia ya mawasiliano katika matukio muhimu yanayowajumuisha wanakijiji wote.SOUND imekuwa ikitumika katika mataifa mbalimbali tangu enzi na enzi kama kiashirio.

TUNAPATAJE SOUND:)-
Tunapata sound-"mlio" kwa kugonga/kupiga kitu chochote,au kutoka kwenye milio 
ya ndege,maji ya bahari,magari na vyombo vingine vya usafiri.
Mashine za viwandani hutoa pia milio ambayo ni milio tu hatuwezi kuiita muziki.Tunaweza kupata sound pia kutoka kwenye vyombo vya muziki vilivyotengenezwa maalum  kwa ajili ya kuutengeneza/kupiga muziki. 

Ni pale tu chombo kinapopigwa na mtaalamu anayekijua,ndipo tunaweza kusema....muziki umesikika kwakuwa,sauti ya kupendeza imeingia masikioni mwetu na kugusa hisia zetu.

TUNAWEZAJE KUTENGENEZA MUZIKI?.
Kwanza ielewekee kwamba si kila mtu anaweza kujiingiza kwenye tasnia hii, 
kwani "kipaji" ni kitu cha kwanza katika kujiendeleza ki-muziki.Muziki ni sanaa inayohusiana na kuufanya mlio ugeuke burudani,ni sanaa ambayo inaweza 
kugeuza sauti zisizo katika mpangilio kama mvumo wa maji ya bahari, kuchanganywa katika muziki uliopangwa na zikasikika kwa namna ambayo
walengwa wataliwazwa.
 mwenye kipaji katika sanaa hii anaweza kukiendeleza kipaji chake kwa kuingia shule ya muziki na kujifunza namna ya kusoma lugha ya wanamuziki ambayo 
kwa kitaalamu inaitwa "STAFF-NOTATION".
Staff-notation ni mchanganyiko wa alama mbalimbali za ki-muziki ambazo
zinajenga lugha ambayo kuisoma kwake ni kuimba kwa kutumia sauti
au kwa kutumia sauti ya chombo cha muziki.

Alama hizo ni kama kitambulisho cha sauti za juu ndani ya chombo cha
muziki,kwa kitaalamu tunakiita "TREBLE CLEF",au "G clef" kwani kitambulisho hiki
kinaanzia kwenye noti ya G.Ukiangalia vyema kielelezo cha hapo chini utaona,
mduara wa treble clef unajizungushia kwenye mstari mwekundu ambayo ni sehemu
tunayopata noti ya G.
au cha sauti za chini
kijulikanacho kwa jina la "BASS CLEF"Bass clef au "F clef" kwani kinaanzia
kwenye noti ya F kama duara la Fclef linavyoonesha.Hivi ni vitambulisho muhimu 
sana kwani vinaziunganisha sauti za juu na za chini za muimbaji au za vyombo
vya muziki,kwa kuitumia noti iitwayo C ya kati (MIDDLE C).Noti za muziki husomwa
ki-alfabeti kama C,D,E,F,G,A,B,C ambayo ni sawa na kusema,DO,RE,MI,FA,SO,LA,
TI,DO.Kwa kifupi hii ni ngazi(scale)  ndani yake tunapata ghani ya nyimbo.
Kisha ngazi inapovunjwa vunjwa katika vipande vipande,hapo tunapata kodi zilizo
vunjwa(broken chords)ambazo husaidia kutengeneza ridhimu ya wimbo.Kutoka 
kwenye DO hadi DO ya juu,tunaita oktava moja(ONE OCTAVE).Vyombo vya muziki
kama Piano huwa na urefu wa octave 5 hadi 6.
Octave ni sauti zinazorudiana kwa kwenda juu au chini.
Middle C and Other LettersKuna alama nyingine kama vile STAVE Musical staff
 ni mistari mitano yenye nafasi 
nne,ndani ya mistari na nafasi hizi kuna noti(NOTES) ambazo zinapangwa kwenye
mistari na nafasi za stave

Noti hizi zinapanda na kushuka kwa viwango vya nusu hatua(SEMI TONE) na 
hatua nzima (TONE).Kuna alama za noti nyingi tu,lakini nitumie noti nne ambazo
ni za msingi.Kwanza ni "noti nzima" yenye umbo la yai( WHOLE NOTE)ambayo ina idadi ya mapigo manne.
Hicho kitofali cheusi ni pigo la kimya(REST) ambalo lina thamani sawa na noti nzima.Noti ya pili ni nusu noti(MINIM )yenye idadi ya mapigo mawili,noti hii ina umbo la
yai tupu lenye mkia upande wake wa kulia.Noti ya tatu ni robo noti(CROTCHET ) yenye
umbo kama la nusu noti ila tofauti yake ni kwamba robo noti tumbo lake lina
giza na mkia kama wa nusu noti upande wa kulia Thamani yake ni pigo moja.
Noti ya nne ni kinane(QUAVER )File:Music-eighthnote.pnginafanana kabisa na robo noti ila mkia wake una alama
ya "kibendera kinachopepea,ikiwa na thamani ya nusu pigo.Pigo lake la kimya
linaonekana na alama kama unavyoiona kwenye chati hapo chini.

Kuna noti nyingi tu lakini katika mada hii nitaishia kuitambulisha noti yenye idadi
ya robo pigo,ambayo kwa kitaalamu tunaiita SEMIQUAVER.Noti hii ni sawa kabisa
na  kinane lakini ina bendera mbili zinazopepea katika mlingoti wake.Tuiangalie
umbo lake.
Bado kuna utitiri wa alama zinazojenga staff-notation ziweze kuimbika kikamilifu
,kama Vipandisho"SHARPS", kama unavyoiona().
 Sharp, hutumika kuipandisha noti na viteremsho "FLATS " kama unavyokiona (♭), hutumika kuishusha noti.Sharp huipandisha noti kwa kiwango cha nusu hatua(SEMITONE)  au hatua nzima(TONE) kwenda juu au chini.
Vilevile Flat huishusha noti katika kiwango cha nusu hatua au hatua nzima.
Pia kuna alama inayoitwa (NATURAL )Naturalsinayofuta alama ya flat au sharp iliyotumika
mbeleni inapotakiwa i-lie kama noti ya kawaida(natural).Utitiri wa alama ni mwingi
lakini kwa mada ya leo,hizi nilizotaja zinatosha.

Hapa nazipanga noti zote zikionekana kwa sura,idadi ya mapigo yake pamoja na
alama zake za mapigo yake ya kimya(Rests) kwenye chati ifuatayo.Mapigo ya kimya
ni muhimu sana katika muziki kwani huufanya wimbo uwe na mlingano uliowiana.
Kila pigo la noti lina pigo lake la kimya kama ninavyoorodhesha kwenye chati hii.

Ndani ya STAVE,vyumba mblimbali hugawanywa kulingana na mwendo(Tempo)
wa wimbo na mapigo yake ili yasizidiane na kuufanya wimbo au muziki uwe katika
uwiano uliolingana sambamba na mapigo.Mlingano huu kwa kitaalamu tunauita
Time signature kama mfano huu unavyoonesha.
Ukijua kusoma na kuandika muziki,inasaidia kutengeneza muziki kwa kuandika
kwa kutumia alama hizi, ambazo zinasomwa katika somo la nadharia ya muziki
(Theory of music).Kujua kusoma na kuandika muziki kunamfanya mwanamuziki
awe na upeo mkubwa katika uelewa wa miziki ya namna mbalimbali duniani.

Mwanamuziki asiyejua kusoma na kuandika muziki,anaweza kutunga wimbo
kwa kutumia hisia na kipaji Mungu alichompandikizia kwenye damu yake lakini....,
upeo wake utakuwa finyu katika kuielewa aina nyingine ya miziki duniani.
Hata wakati wa kukopi nyimbo,kuna baadhi ya nyimbo ambazo zimetungwa kwa 
kutumia utaalamu wa juu kwa mfano miziki ya jazz au classic ambayo watunzi
wake hutumia ufundi na utaalamu wa kisomi kuitengeneza.

Miziki ya aina hii haiwezekani kuikopi kwa kutumia masikio pekee,ina utaalamu
mwingi wa kisomi katika tasnia ya uandishi wa muziki.Kujua kusoma muziki ni
nyongeza itakayomuwezesha mwanamuziki "kuelea" ndani ya anga ya muziki
popote duniani,ingawa pengine anaweza kuikosa "feeling" halisi.

Mfano mzungu ajuaye kusoma na kuandika muziki,apewe noti zilizoandikwa
 muziki wa kiutamaduni wa Wagogo.Haiyumkini,ataweza kuupiga lakini hawezi k
uupiga kama mgogo mwenyewe kutokana na kukosa "feeling".Cha muhimu
hapa ni kwamba "angalau atajitahidi.Lakini kwa asiyejua kabisa kusoma na
kuandika muziki,atanawa mikono na kushindwa kabisa kuusoma muziki ulioandikwa.

Wanamuziki waliokosa elimu ya muziki ,huweza kupiga miziki iliyo katika mahadhi ya maeneo ya nchi  walizokulia.Kusikia miziki ya aina fulani tangu utotoni,kunamjengea mwanamuziki mazingira ya uwepo wa milio ya miziki hiyo katika nafsi yake.
Kitu ulichozoea kukisikia tangu utotoni,ni rahisi kukifuatisha kama kipaji kipo hata
kama husomi na kuandika muziki.

FUNGUO(KEYS ) NA CHORD (KODI) ZA MUZIKI.
Funguo zinafanya wanamuzuki waweze kupiga muziki wakipita kwenye mstari
mmoja.Funguo ni kama barabara inayowawezesha wanamuziki kuendesha
gari lao(muziki) juu yake.Funguo ni kipimo cha kiwango cha sauti iliyo chini na 
iliyo juu.
Kwa mfano waimbaji wenye kuimba sauti za juu,hupendelea key za juu kulingana
na uwezo wa sauti zao.Waimbaji wenye sauti nzito,huchagua key za chini ili wasikwame wakati wanapoimba sehemu iliyo juu katika wimbo.

Chord hutumiwa zaidi na wapiga vyombo ili kuufanya wimbo usikike na uzito.
Chord moja inaweza kuwa na idadi ya noti tatu hadi nne zinazopigwa kwa pamoja
ili kumjengea muimbaji mazingira mazuri katika uimbaji wake.Chord huonekana
kama hivi.

Kuna Chord za namna nyingi kutegemeana na uamuzi wa mtunzi,Chord zinaweza
kuubadilisha wimbo mbaya ukasikika vizuri masikioni.Chord zinaweza kuufanya
wimbo uwe wa huzuni au wa furaha.Ili kuufanya wimbo uwe wa huzuni,tunatumia
kodi zinazoitwa "minor chords" au kodi ndogo.Kuna aina nyingi ya kodi zinazotumika kulingana na melody(ghani) ya mtunzi.

Kuna kodi zilizoongezwa(augmented chords),kodi zilizopunguzwa(diminished chords),kodi ndogo za seventh  zilizoongezwa flat katika noti ya 5(minor
 seventh flat 5),au kodi kuu ambazo noti ya tano inawekewa alama ya flat(major
seventh flat 5).Kuna kodi kuu na ndogo za kawaida.Hili ni somo pana sana ambalo
linamchukua mwanafunzi wa muziki miaka kadhaa kabla ya kujua kodi zote
na namna ya kuzitumia katika chombo chake.

VYOMBO VYA MUZIKI NA MAKUNDI YAKE.
Vyombo vya muziki vimetengenezwa na kugawanywa katika makundi manne makubwa,makundi haya yanagawanywa kulingana na nini kinachokiwezesha
chombo kutoa mlio wake.
Kundi la kwanza ni STRINGS INSTRUMENTS-vyombo hivi vinategemea NYUZI
ili tupate sauti zake,kama vile gitaa na violin kama unavyoona picha.violin 

Kundi la pili linaitwa "MEMBRANOPHONES"-hivi ni vyombo vinavyotegemea sana "mtetemo wa NGOZI ili viweze kutoa sauti zake,Wengine huita "Percussion".
Ngoma za namna zote au hata drums inayotumika sana kwenye muziki wa dansi inapatikana kwenye kundi hili.
                      Kundi la tatu linaitwa "IDIOPHONES" au kwa kiswahili chepesi ni vyombo vya kugongwa kama kengele,marimba nk.
Kundi la mwisho linaitwa "AEROPHONES"-hivi ni vyombo vinavyotumia hewa
ili vitoe sauti yake.Saxaphoni,filimbi,tarumbeta na vinginevyo vinaangukia kwenye kundi hili.
Kila chombo kimetengenezwa tofauti na namna ya kujifunza ni tofauti,ingawa vyote
vinatoa sound na vinaweza kupigwa kwa pamoja katika bendi kubwa yenye
wanamuziki wengi yaani "ORCHESTRA".

Mpigaji wa chombo hiki si lazima awe anajua na kile kwani mazingira ya kujifunza
ni tofauti kabisa.Kwa leo nimeona haya machache yanaweza kuwa msaada kwa
yeyote anayependa kujifunza japo mawili matatu kuhusiana na tasnia hii.
Siku zijazo nitaendelea na sehemu ya pili ya mada hii,ambapo tutaingia ndani zaidi,
kujifunza mwendo wa mapigo na alama nyingine za muziki.

Mwandishi wa makala hii anaitwa Lister Elia,yeye ni Pianist na ni mwandishi
wa vitabu vya PIANO,JIFUNZE GITAA na kitabu cha riwaya kiitwacho "The mystery
 of Tamko's death".
Kama mwanamuziki wa kulipwa,anashiriki katika matamasha mbalimbali ya muziki
wa Jazz na muziki wa Afro-pops,akiitangaza Tanzania kama video yake hii inavyoonesha.

 

Anaishi Tokyo Japani,akifanya kazi kama mwanamuziki wa kulipwa na kuandika 
vitabu.Hutumia muda wake wa ziada  kufundisha muziki katika vyuo mbalimbali vinavyojihusisha na taaluma hii nchini Japani.

LISTER  ELIA'S  NEW  BOOK  IN  PROGRESS!.
 
PROLOGUE.
A  new book(novel) by the title  "TAMKO" is in progress.TAMKO represents TALANTA  MULOKOZI  KOTAISINGWA, a popular name  in Bukoba town in the North West province of Tanzania, near the famous Lake Victoria. TALANTA MULOKOZI KOTAISINGWA was a school mate at Kibaha Secondary school. His name was too long to pronounce, no wonder we shortened it to TAMKO. TA represents  TALANTA, M stands for MULOKOZI and KO represents KOTAISINGWA. TAMKO had a big dream in his life, and his dream was to become the wealthiest man in his land. TAMKO's passion for wealth drove him to go beyond overlooking education. 

To TAMKO, studying at the Primary or Secondary school was just a  waste of time!. He therefore didn't spend a lot of time reading like other children would do, instead, TAMKO engaged secretly in small businesses of various kinds like selling of sweets,ciggarates,pencils,and pens among others. He had to do so since it was against the schools rules and  regulations. TAMKO later decided to drop out of secondary school after being warned several times by the school's management. He therefore ended up as a street vendor where he specialized in the sale of small items in the streets of Dar-es-salaam. It was while in that business that he met mr  Nawaz, who described himself as a Tanzanian of Pakistan origin. Nawaz made friendship with TAMKO and managed to recruite TAMKO into illegal business. 

TAMKO knowingly or unknowingly carried sales of illegal drugs. To TAMKO this suited him so well since he could make quick deals in a short time.  Nawaz agenda was however different and so he arranged for a proper training in Pakistan.This made TAMKO so famous since he acquired the right skills to sell drugs from one country to another. It took only months and TAMKO was qualified enough to dodge police men and immigration officers during  his trips to Pakistan, Afghanistan, Kenya, America, europe and the Far East. Within a year and half TAMKO became a fabulous wealthy man and returned to his native country where he started his own company. 

TAMKO changed tricks and got himself to sell big items like brand new cars to small items  like match boxes, of course under cover. While his business expanded faster and he became very famous, TAMKO was murdered in mysterious circumstances in Nairobi ,Kenya, a neighboring  foreign country.His body was mutilated and cut into pieces. You could hardly have recognized him. Who killed TAMKO? why would the killers go after TAMKO and end his life in a foreign country? Was it possible for the killer or killers to be brought to books? will justice prevail for TAMKO? Did TAMKO deserve to die or was innocently murdered? What was the aftermath of his death?. Find out all this and  much more from Lister Elia thrilling novel TAMKO to be released soon. This is a story full of imagination though some of the parts depict the writer. You cannot miss out on this one on the bookshelves!. To all my fans, and lovers of music around the globe, to whom i truly dedicate and hope that  you will enjoy reading TAMKO and find out the other side of Lister Elia.

'JIFUNZE GITAA'"Jifunze Gitaa" .Is one of the books that i wrote a few years ago as my first finger works. My aim was to help those people who would like to learn how to play the guitar. Though i trained as a pianist, i have learnt over time many aspects about music right from when i was at the Music School and  during my career life. This includes music history,conducting music,music theory,how to play the trumpet,guitar,recorder and other music instruments. I therefore acquired good knowledge that i would willingly like to share with other people in the world who probably didn't get the chance like i  did, no wonder i wish to write more and more books!. I believe it's easy to carry the guitar wherever and play anywhere. Infact, a guitar belongs to the class of instruments classified as "chordophones" though it can also be used as a leading instrument. For more information please check  information file.
 

'PIANO'"Piano" is a kind of text book designed to teach people who wants to learn how to play the piano but they failed to do so due to lack of piano teachers especially in developing countries like Tanzania where music isn't officially included into school's syllabus. 
It was my dream since my boyhood to  write a manuscript and share whatever i have with my fellow musicians or anybody who wants to learn how to play the piano.
"Piano" is written in a very simple(swahili)language & it's easy to understand. 
You can learn basic technics in a very short time & you can make your own sound and develop as you like. It's helpful even for those who wants to read without engaging themselves into practical cus it has a wide range of musical history, theory and alot of things unrelated to practical. For more information.. check  information file p/s!.

THIS SPEECH PREPARED AND DELIVERED BY LISTER ELIA AT CHIBA UNIVERSITY.
2006.02.2nd

Africa, to most people is a unknown continent.       
And for those who tend to have alittle knowledge of africa they know nothing but negativity and the dark side of the continent. Wars, aids, malaria, refugees, poverty, street children, tribalconflicts, corruption is the image of most people.
The strongest images of Africa are savanna traversed by animals such as the zebra and lions, jungle INHABITED by roving bands of mountain gorillas.
Indeed this has been the works of mass media from news papers to Television  broadcasting programs here in japan to mislead the people by spending most of their time writing and showing mostly the dark side of Africa.While Africans living in this country do not seem to care about taking the bad side of japan like japan's past history that caused so much pain and suffering to other neighbouring countries,or the issue of japanese homeless to their own people in Africa as the
image of japan.
Instead,most africans are trying their level best to learn good side of japanese people in terms of technology, economical to build their continent for the better.
Africa's diversity and vastness surpass such images. From Egypt to South africa,Madagascar to Nigeria there is alot to talk about development,culture,trade,agriculture,science,economic
strategy,politics,and international relations. Africa was divided and colonized by europeans and that left some scars that Africa needs to work hard to overcome the effect of the so called
DIVIDE AND RULE. The ideology did srengthen tribalism that mostly causes wars in africa
.While the so called five permanent members of the United Nation England,France,China,Russia and the United states of America enjoying by selling arms to both corrupt  African goverments and to the rebels who wants to take over and continue with their personal agendas. A dacade ago, massacre happened in Rwanda  between the main tribes of Tutsi and Hutu. More than a million people died in a short period of time and the so called permanent members of the United Nations and other developed
nations could only sit back and watch what was  going on.
Africa is scattered by KALASHNIKOV(a russian famous gun)mines and other dangerous weapons.
From Mozambique to Liberia,Eritrea to Somalia gun running has been a disaster to most Africans.
A place like Darfur in Sudan, refugee camps are every where because of the unfolding events between Sudanese government supporting the muslim janjaweed rebels to  discriminate blacks of western sudan. Burning villages,killing people and  raping women has been the subject of daily life in darfur despite the involvment of UN there.
Africa is very rich in terms of natural resourses like diamonds,oil fields,gold,the tanzanites and other precious stones but politicians,corrupt leaders and bad contracts are the main problems hindering development from this natural resourses.
Despite all this problems Africans are moving fast into the world of technology and communication.
Free market system is widely used almost everywhere in Africa and thus making it easier for normal Africans  to buy whatever they want in their  own countries. Internet caffee are everywhere  and people can gain access to the internet and  communicate with their loved ones wherever in the world.
Some African countries economies is  booming like a flower Agriculture is the main source of income to most Africans. Countries like Uganda,Kenya and Tanzania are the main coffee and tea
producers in Africa. Ghana and other west african countries produces KAKAO  COCOA and
CHOCOLATE.Countries like Tanzania also produces sisal,maize,groundnuts,cassava and many more.
Bad news is that....the price of African tea  and coffee is always controlled by developed rich countries and thus Africans end up selling alot  but receiving small amount of money.
AFRICAN MUSIC. We have two different kinds of African music.
We have TRADITIONAL AFRICAN MUSIC and AFRICAN MODERN MUSIC.
When we play tradition music mainly we use traditional instruments  like Marimba,kalimba,tradition drums and many more. Just like Western musical instruments,african traditinal instruments
are divided into 5 different groups. We have strings instruments,Idiophones,membranophones, wind instruments and chordophones instruments. I want to elaborate and emphasize about few things here that basically African traditional music does not have chords like western music.
There is no way you can find full  minor chord,minor melodic,augmented  chords,major seventh,minor seventh,or diminished chords. There is no way you can find a major western scale into African
Traditional music. Traditional  music is based into TRIBAL PENTATONIC SCALES.(elaborate
more about pentatonic). MODERN AFRICAN MUSIC.
When we play modern African music western musical instruments like keyboards,guitars,trumpets,saxophone can be used and normal western scale.We  simply call  AFRICAN POPS. This two types of music is always rythmic and danceable.
AFRICAN CULTURE. African culture also depends on tribal structure and religion.
The main religions in Africa are christians and muslims. But most Africans have somethings in common like to get  all baby boys CIRCUMCIZED before they become adults.
Women circumcission is also common to some tribes though it has been critisized by scientists and womens right societs around  the world. Men circumcission is a common practice in the Arab world , middle east and parts of Europe as well.Africans does same kind of ceremonies during
birth,funerals and festivals. Every tribe has it's own culture,own language and thus making it
possible for most Africans to speak more than one language.
                   
TANZANIA.
Africa is a continent that contains  53 countries and Tanzania is oneof them.
Geographic,Tanzania is in the eastern part of Africa.
The main city is Dar-es-salaam which lays in the coastal area of an Indian ocean.It has  120 different tribes but people speak swahili and english as the main languages. It was under british colonial rule until Dec 1961 when she gained independence.
Tanzania is surrounded by three great lakes.Lake victoria(the biggest in Africa),lake Tanganyika(the deapest in Africa) and lake nyasa. She has the most beautiful parks where animals and birds can be found. Ngorongoro crater,serengeti,and selou is one of the most famous tourists destinations for folks from all over the world.
Mount kilimanjaro  at 5,896 meters is the highest mountain in Africa
and it is also a tourist destination.
Tanzania has alot of minerals like diamonds and the Tanzanites a
precious stone that can be found only in Tanzania .
The population is about 38 million  people.
Zanzibar also is a nice place to visit filled with tourist attraction.
Main food is rice  for those who lives in the coastal  areas and UGALI
a kind of hot bread made by maize flour for those who lives in the mainland.
Tanzania is the place where a skull  of the first and  oldest human being was found in olduvai Arusha by Dr  Livingstone.
Tanzania is the main speaker of swahili language and the result of that more than six countries in Africa use this language as one of their languages.Swahili is the biggest spoken language in Africa. There are many japanese scientists in my country making research about various issues like forest creatures.
We have so many japanese companies there doing business with our country like KAJIMA,MATSUSHITA ELECTRIC COMPANY,KONOIKE and many more.
Believe me or not almost 80% of all cars in Tanzania are japanese cars made by japanese industries.
So you can just figure out by yourself the magnitude  of business between  this two countries.
LANGUAGE SIMILARITY.
There is alot of similarity between swahili and nihongo.Like MIMI,NANI,YUKO,(Fresh will say something).                     
TANZANIAN FOOD.
Tanzanian food is  very much influenced by indian way  of cooking.You can always find fresh food,meat,fish,potatoes,vegetables,fruts like mangos,passion fruits,pinaples,apples,guava,oranges always available and fresh. People can eat many more tropical fruits.
  SPORTS ACTIVITIES.
Soccer is probably the most famous sport in Tanzania  followed by boxing, athletics like marathon runners,netball and other sports. Juma Ikangaa is one of the most famous Tanzanian marathon runner here in Japan he won TOKYO MARATHON competitions here in japan  a couple of
years ago. Sports like baseball, sumo,kendo,figure skating,gymnastic,ski and other
winter sports is widely unknown in Tanzania and probably many parts of Africa.
TANZANIA EDUCATION SYSTEM.
 We have seven years of primary education in Tanzania  followed by 4 years of secondary school,two years high school education and three or four years university  education this depends on majors.
We have alot of technical schools where people can learn various studies inorder to help and build their nation. Primary education  is free and every kid is eligible to primary education.
A couple of years  ago Tanzania was  leading in Africa in terms of a number of adults who knew how to read write. It was a campain led by Tanzanian Government to make sure that those adults who for some  reasons missed primary school education especially elderly people from rural areas they could learn how to read and write so that they could have  the opportunity to fully participate to build
their country.
 PEACE.
For centuries Tanzania is well known as a country of peace.perhaps because of those who used to rule the country even before colonialism. Despite having 120 different tribes,there is no tribal conflicts for
centuries. People from north  to south,west to east live together.It's a common practice for Tanzanians to marry someone from a different tribe and even religion.
Because of the sense of freedom,togetherness and peace, Tanzanians helped many African countries gain independence from brutal colonial rule.

Tanzanians helped countries like Mozambique,Zimbabwe,South Africa to
gain independence. As we speak there are so many refugees  coming from  unstable countries
 like Rwanda,Burundi and  Democratic Republic of Congo where tribal conflicts, corrupt politicians and rebels causes trouble in the region. The number of refugees is always going up and causes trouble to normal Tanzanians because of crimes commited by refugees, some of them
bringing guns and other weapons with them. Alot of refugees entering through Tanzania borders illegally are causing trouble for the government of Tanzania to separate the "good and bad apples" because some of those refugees are soldiers or rebels running away to escape fighting  in their own countries. The problem of children-soldiers  makes  even more difficult for the government to neutralize  the situation due to a big number of children-soldiers crossing Tanzanian borders..
Nevertheless Tanzanian government is always neutral into civil wars  of  its neighbour and  the goverment of Tanzania respects human rights and all resolutions of the United nations.
So refugees are always treated well  regardless how they entered as long as they do not commit crime while staying in Tanzania.
LAST WORD.

We just want to congratulate you for reaching the end of your term and as you prepare to start a new semester,always remember A FALL IN A PIT IS A GAIN IN YOUR WIT. Adjusting to a new thing is always tough. If there are somethings that went wrong,you have to rectifie them so that you will be able to start a new term with a new strategy. BE HUMBLE TO OTHERS,ADDRESS YOUR PRESENCE AT THE SAME TIME SHOWING VIVIDLY YOUR PERSONALITY.
Finally,always remember that,FAVOURS AND FRIENDS ARE LIKE MONEY IN THE BANK...ALWAYS READY FOR EMERGENCIES  IF NEED SHOULD ARISE. Making friends and good understanding with people will trigger peaceful life that will no doubt lead to a successful career for you guys.GOODLUCK AND GODBLESS.